SEOUL : Ameahidi kutatuwa mzozo wa Korea Kaskazini | Habari za Ulimwengu | DW | 11.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SEOUL : Ameahidi kutatuwa mzozo wa Korea Kaskazini

Katibu Mkuu mteule wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema atatumia ushawishi wake kusaidia kutatuwa kwa njia ya amani mgogoro wa nuklea wa Korea Kaskazini.

Ban ametowa kauli hiyo katika bunge la taifa mjini Seoul wakati alipokuwa akin’gatuka rasmi kwenye wadhifa wake wa waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini.

Pia ameapa kuendeleza mageuzi ndani ya Umoja wa Mataifa na kushughulikia masuala ya dunia kama vile ugaidi na umaskini.

Ban anachukuwa nafasi ya Kofi Annan ya Ukatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hapo Januari Mosi mwakani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com