Sarkozy atakuwa rais mpya wa Ufaransa | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 07.05.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Sarkozy atakuwa rais mpya wa Ufaransa

Tangu jana usiku, matokeo ni wazi: Wafaransa wamemchagua rais mpya. Jina lake ni Nikolas Sarkozy, mgombea wa chama cha kihafidhina, ambaye alikuwa waziri wa ndani. Kama livyokuwa kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi wiki chache zilizopita, idadi ya watu waliokwenda kupiga kura ilikuwa kubwa sana.

Nicolas Sarkozy

Nicolas Sarkozy

Wafuasi wake wanaimba Nicolas, Nicolas, wakimshangilia mshindi wa uchaguzi huu. Wanapepeya bendera ya Ufaransa na maputo yenye rangi ya buluu ambayo ni rangi ya chama tawala cha kihafidhina. Akipata asilimia 53 ya kura, Nicolas Sarkozy alichagulia kuwa mrithi wa rais wa sasa Jacques Chirac.

Ni kama ndoto iliyogeuka kuwa kweli, alisema Sarkozy: “Ninaipenda Ufaransa ni ikiwa kiumbe ambaye imenipa yote. Sasa ni zamu yangu kurudisha yote niliyopewa.”

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya ushindi wake ulipotangazwa, Sarkozy alitaja pia yale ambayo anataka kuyabadilisha nchini Ufaransa ili Wafaransa wajivunie tena kuwa Wafaransa. Lakini Sarkozy hakubakia kwenya siasa za ndani tu, bali pia alizungumzia sera za kuelekea nje akisisitiza hasa umuhimu wa Umoja wa Ulaya: “Maisha yangu yote nimejisikia kuwa mtu wa Ulaya. Nataka Ulaya ijengwe vizuri na kuanzia leo usiku Ufaransa imerudi barani Ulaya.”

Katika pongeza zao, viongozi wa serikali ya Ujerumani walitaja matumaini yao kuwa rais mpya Sarkozy atasaidia katiba ya Umoja wa Ulaya ipewe umuhimu tena.

Wakati huo huo, Sarkozy alionya kuwa Umoja wa Ulaya unapaswa kuzingatia wasiwasi wa mataifa yake katika enzi ya utandawazi. Nchini mwake, Sarkozy atakabiliwa na changomoto chungu nzima. Katika sekta za uchumi na ajira, Sarkozy anapanga kutekeleza mageuzi. Deni la taifa hivi sana ni kubwa mno. Hapo Wafaransa walimuamini Sarkozy kuwa na uwezo zaidi kuliko mshindani wake mgombea wa chama cha Soshialisti, Segolene Royal.

Bibi huyu, kwa upande wake, mara tu baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa, alikubali kushindwa na kumtakia kila la heri rais mpya. Bi Royal aliahidi kufanya mageuzi katika chama chake cha mrengo wa kushoto ili kuhakikisha ushindi katika uchaguzi wa bunge utakaofanyika mwezi ujao.

Wapinzani wengine wa Nicolas Sarkozy lakini hawakutaka kukubali rahisi hivyo. Muda mfupi tu baada matokeo kuarifiwa, kulitokea fujo na ghasia katika miji kadhaa. Jijini Paris, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na mabomba ya maji kuwatawanya maandamanaji takriban 2000. Kwa mujibu wa polisi, katika ghasia hizo tangu jana usiku, zaidi ya magari 360 yalitiwa moto na watu 270 walikamatwa.

 • Tarehe 07.05.2007
 • Mwandishi Maja Dreyer
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB4I
 • Tarehe 07.05.2007
 • Mwandishi Maja Dreyer
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB4I
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com