Robert Mugabe atagombea tena uchaguzi wa rais Zimbabwe | Habari za Ulimwengu | DW | 14.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Robert Mugabe atagombea tena uchaguzi wa rais Zimbabwe

HARARE: Chama tawala nchini Zimbabwe ZANU-PF kimemchagua Rais Robert Mugabe kugombea uchaguzi wa rais mwaka 2008.Hatua hiyo itamruhusu Mugabe kubakia madarakani kama rais kwa miaka mitano mingine. Mugabe anatawala nchini Zimbabwe tangu nchi hiyo kujipatia uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1980. Alipohotubia mkutano wa chama mjini Harare, Mugabe alitoa mwito kwa wafuasi wake kutotumia nguvu dhidi ya wapinzani katika kipindi kinachotangulia uchaguzi huo.

Mapema mwaka huu,viongozi kadhaa wa chama kikuu cha upinzani MDC walishambuliwa na kupigwa vibaya vikosi vya usalama vya Rais Mugabe.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com