Rajoelina atangazwa rais wa mpito nchini Madagascar | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 18.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Rajoelina atangazwa rais wa mpito nchini Madagascar

Jeshi limemuidhinisha rasmi kiongozi huyo baada ya rais kujiuzulu

''Kiongozi wa upinzani Rajoelina akiwapungia mkono wafuasi wake mjini Antananarivo''

''Kiongozi wa upinzani Rajoelina akiwapungia mkono wafuasi wake mjini Antananarivo''

Wakuu wa kijeshi nchini Madagascar wamesema wamemuidhinisha rasmi kiongozi wa upinzani Andry Rajoelina kuwa rais wa kipindi cha mpito nchini humo.

Hatua hiyo imekuja saa chache baada ya rais Marc Ravalomanana kutangaza kujiuzulu na kulikabidhi jeshi madaraka.

Upinzani unamshutumu rais huyo kwa utawala mbaya wa kisiwa hicho.

Zaidi ya watu 100 waliuwawa katika maandamano na ghasia tangu kuanza mzozo huo wa kisiasa mwaka huu.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ametoa mwito kwa vyama vyote kubeba jukumu na kurudisha demokrasia nchini humo.

Baraza la usalama na amani la Umoja wa Africa pia limetoa taarifa yake na kugusia juu ya kujiuzulu kwa rais Marc Ravalomanana na kutaka katiba ya nchi hiyo iheshimiwe.Mwandishi: Saumu Mwasimba/ZR

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com