Rais wa Zamani wa Czech amefariki dunia | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.12.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Rais wa Zamani wa Czech amefariki dunia

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Czech na mpinzani, Vaclav Havel, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75. Tovuti ya Gazeti la kila siku nchini humo, Dnes, ilimnukuu msemaji wake wa zamani, akitangaza hayo.

File - In this Oct. 15, 2009 file photo former Czech President Vaclav Havel is seen during a press conference on occasion of the 20th anniversary of the changes in Czechoslovakia and the fall of the Iron Curtain in Prague. Havel, the dissident playwright who wove theater into politics to peacefully bring down communism in Czechoslovakia and become a hero of the epic struggle that ended the Cold War, has died. He was 75. (AP Photo/Petr David Josek)

Rais wa zamani Vaclav Havel

Vaclav Havel alifanyiwa upasuaji 1996 kutokana na saratani ya mapafu, na alikuwa akitibiwa ugonjwa unaotokana na shida ya kupumua. Kiongozi huyo alikuwa mmoja kati ya watu muhimu sana katika harakati za Ulaya Mashariki kuupindua mfumo wa siasa za kikoministi na kuja kipindi cha mpito kuelekea demokrasia. Mtunzi huyo maarufu wa michezo ya tamthilia, mpinzani na mwanaharakati wa kuupinga utawala wa kikominsti katika iliokuwa Czechoslovakia, baadae alikuwa rais baina ya mwaka 1989 hadi 1993, na baadae kama mkuu wa jamhuri mpya iloundwa ya Cheki hadi mwaka 2003.

Mwandishi Sudi Mnette

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com