Rais wa Israel amejiuzulu | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Rais wa Israel amejiuzulu

Rais Moshe Katsav wa Israel amewasilisha hati za kujiuzulu wadhfa wake kufuatia tuhuma za kuwadhulumu kimapenzi wafanyakazi wake kadhaa katika ofisi yake.

Rais wa Israel aliejizulu Moshe Katsav

Rais wa Israel aliejizulu Moshe Katsav

Kwa mujibu wa radio ya taifa nchini Israel rais Moshe Katsav amewasilisha hati zake za kujiuzulu kwa spika wa bunge la Knesset, Daila Itzik.

Hatua aliyochukua rais Katsav ni miongoni mwa maamuzi magumu aliyohitajika kuyafanya baada ya makubaliano na mkuu wa sheria wa Israel.

Katsav mwenye umri wa miaka 61 na mzaliwa wa Iran hapo,jana alitia saini mlolongo wa tuhuma za dhuluma za kimapenzi dhidi yake ikiwa ni pamoja na unyanyasaji na utovu wa nidhamu.

Lakini licha ya makubaliano yaliyokuwepo baina ya rais huyo aliyejiuzulu na mkuu wa sheria wa Israel hii itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo kwa kiongozi kuwahi kushtakiwa kwa makosa ya dhulma za kimapenzi.

Katika kipindi cha saa 48 spika wa bunge Daila Itzik ataidhinishwa kuchukuwa wadhfa wa rais wa mpito na hapo kuamrisha serikali imfungulie mashtaka rasmi rais Moshe Katsav aliyejiuzulu.

Katika muda wa wiki mbili kipindi chake cha miaka saba kitakuwa kimekamilika na hapo kumpisha mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Shimon Perez kuchukua madaraka ya kuiongoza Israel baada ya kushinda katika uchaguzi wa rais uliomalizika mwezi jana.

Bwana Shimon Perez atakuwa rais wa tisa wa Israel.

Katika makubaliano yaliyofikiwa rais aliyejiuzulu Moshe Katsav amekiri adhabu ya kifungo iliyoodhoshwa dhidi yake na faini ya dola elfu kumi na moja za fidia lakini wakati huo huo aemkwepa adhabu nyiyngine ya kifungo iwapo atapatikana na hatia ya ubakaji.

Watetea haki za wanawake na vyombo vya habari nchini Israel wamelaumu juu ya makubaliano hayo na kutaja kuwa yanakiuka haki na sheria za nchi hiyo.

Mwanzoni mwa mwezi Mei rais Moshe Katsav aliyejiuzulu hakutaka kabisa kukubali kashfa hiyo dhidi yake.

Alijitetea kwa juhudi zote na hata kuwaambia wananchi kuwa yote hayo yalikuwa masingizio yaliyolenga kumuharibia jina.

Bwana Katsav aliwahi kusema, wananchi msiamini masengenyo na uongo, hakuna ukweli wa aina mbili bali ukweli ni mmoja tu.

Mimi nakabiliwa na kashfa ya fitina za kisheria ambayo ni mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini Israel.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com