Rais mpya wa Urusi Dmitry Medvedev kuapishwa rasmi Jumatano, tarehe 7 Mei. | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.05.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Rais mpya wa Urusi Dmitry Medvedev kuapishwa rasmi Jumatano, tarehe 7 Mei.

Ni nani atakayekua na madaraka zaidi yeye au Waziri mkuu Vladimir Putin ?

Vladimir Putin(Kulia) akiwa na rais mteule Dmitry Medvedev.

Vladimir Putin(Kulia) akiwa na rais mteule Dmitry Medvedev.

Wanachojiuliza wachambuzi ni kwa mfano kuna zuka mgogoro wa kimataifa na viongozi wa kundi la mataifa manane yalioendelea kiviwanda yanayojulikana kama-G 8 wanataka kuzungumza moja kwa moja na Urusi, jee wazungumze na nani , rais Dmitry Medvedev au Waziri mkuu Vladimir Putin ?Kwa mujibu wa katiba Putin hakuweza kugombea tena baada ya mihula miwili ya miaka 4 kila mmoja.

Wanabalozi watalazimika kutathimini hali itakavyokua kwa sababu mara tu Jumatano ijayo atakapoapishwa rais mpya, Urusi itakua na viongozi wawili.

Medvedev mwenye umri wa miaka 42 atakua na madaraka yote kama rais, lakini Putin mwenye umri wa miaka 55 ambaye Medvedev ni chaguo lake, atakua waziri mkuu na kiongozi wa chama kikubwa bungeni na hivyo kukiongoza chombo cha msingi wa madaraka na hivyo anaweza kuwa mtoaji maamuzi mkubwa.

Wakiulizwa panapozuka hali ya dharura watampigia simu anani, maafisa wawili wa ngazi ya juu kutoka serikali ya nchi moja mwanachama wa kundi la G8 waliokua ziarani Moscow mwezi uliopita, walitazamana na baadae mmoja kumjibu mwandishi habari muhusika" pengine wewe unaijua hali vyema zaidi kuliko sisi"

Suala la nani mwenye usemi ni muhimu kwa sababu Urusi haina desturi ya kugawana maadaraka. Wadadsisi wanasema kunaweza kukazuka mtafaruku jambo ambalo litalifanya taifa hilo kubwa la kinuklea lishindwe kutawalika. mmoja alisema inaweza kutarajiwa kwamba panapozuka tafauti ya maoni kati ya Medvedev na Putin kutazuka mgogoro wa kisiasa.

Ni kipi kitakachokua tafauti na waliotangulia kama mawaziri wakuu , pale Putin atakaposhika wadhifa huo, wakati alipokua yeye rais kwa kipindi cha miaka minane ulishikwa na watu ambao hawakua na usemi wowote ?

Chama chake United Russia-Urusi ilioungana- kina wingi mkubwa bunge na kwa hivyo anaweza kuzuwia baadhi ya maamuzi ya Ikulu, kubadili katiba na hata kupitisha uamuzi wa kutokua na imani na rais. Ikumbukwe Putin ni maarufu , wakati Medvedev wakati wote hakua mtu mwenye kujulikana sana katika utawala wa Putin.

Wachambuzi wanasema hana nguzo ya kisiasa, na hivyo hatokua na chaguo jengine isipokua kukubaliana na kitakachosemwa na Putin.

Kwa sasa dhana moja wapo ni kwamba mbali ya picha za Medvedev kuanza kutundikwa katika kuta za maofisi mara atakapokaa Ikulu, Putin anapanga kumuachia mrithi wake aendeshe mambo kivyake ikiwa ni pamoja na kutekelezwa mageuzi na kutoujongelaea kwa kasi upande wa magharibi. Lakini wengine wanasema, hakuna kitakachobadilika, Putin atabakie pekee kwenye usemi wa mwisho . Ni wakati utakaotoa sura halisi ya nguvu za kiutawala nchini Urusi chini ya rais mpya Dmitry Medvedev.

 • Tarehe 05.05.2008
 • Mwandishi Mohammed AbdulRahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DtxY
 • Tarehe 05.05.2008
 • Mwandishi Mohammed AbdulRahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DtxY
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com