1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush asaini muswada wa sheria kuokowa masoko ya fedha Marekani

Mohamed Dahman4 Oktoba 2008

Rais George W. Bush wa Marekani ametia saini kuwa sheria muswada wa mpango wa dola bilioni 700 kuokowa masoko ya fedha ya Marekani.

https://p.dw.com/p/FTuD
Rais George W. Bush wa Marekani.Picha: AP

Hapo jana Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani lilipiga kura kuunga mkono mpango huo wa uokozi uliofanyiwa marekebisho baada ya kuukataa ule wa mwanzo hapo Jumatatu.

Bush amelipongeza bunge kwa juhudi zao za kizalendo na kupitisha muswada huo kwa haraka.

Bush amesema kwa kukubalina juu ya muswada huo wamechukuwa hatua ya kijasiri kusaidia kuzuwiya mgogoro katika soko la hisa la Wall Street kugeuka kuwa mgogoro katika jamii nchini kote Marekani na kwamba wameionyesha dunia kuwa Marekani itayatuliza masoko ya fedha yasiyumbe na itaendelea kutimiza dhima kuu katika uchumi wa dunia.

Mpango huo mpya unajumuisha dola bilioni 150 kwa msamaha wa kodi na kuruhusu serikali kununuwa mali za benki zenye matatizo ambazo zimechochea mgogoro wa fedha katika soko la hisa la Wall Street mjini New Marekani.