QUITO: Waziri wa Ulinzi wa Ecuador afariki dunia kwenye ajali ya helikopta. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

QUITO: Waziri wa Ulinzi wa Ecuador afariki dunia kwenye ajali ya helikopta.

Waziri wa kwanza wa ulinzi mwanamke wa Ecuador, Bibi Guadalupe Larriva, amefariki kwenye ajali ya helikopta siku tisa baada ya kuteuliwa kuwa waziri.

Maafisa wa kijeshi pamoja na serikali wamesema waziri huyo na binti yake walifariki jana baada ya helikopta mbili kogangana.

Ajali hiyo ilitokea karibu na kituo cha kijeshi kwenye pwani ya bahari ya Pasifik.

Bibi Guadalupe Larriva alikuwa mmojawapo wa mawiziri maarufu zaidi kwenye serikali ya Rais Rafael Correa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com