Polisi yakamata gari lenye silaha na picha za kampeni | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Polisi yakamata gari lenye silaha na picha za kampeni

Polisi ya Kenya hapo jana imelibamba gari lenye nambari za serikali lililosheheni silaha na picha za kampeni za Rais Mwai Kibaki.

Naibu kamanda wa polisi wa polisi wa mkoa amesema wamegunduwa mapanga,upinde na mishale pamoja na viboko kutoka kwenye gari hilo katika kizuizi cha barabarani karibu na mji wa mkoa wa Rift Valley wa Naivasha kama kilomita 90 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi.

Kwa muijbu wa afisa mwengine wa polisi aliyekataa kutajwa jina lake mtu fulani mjini Nairobi alikuwa akiujuwa mpango huo mzima na kuwagutusha polisi baada ya gari hilo kuondoka Nairobi .

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com