Polisi wa Urusi waandama wapinzani | Habari za Ulimwengu | DW | 25.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Polisi wa Urusi waandama wapinzani

Saint Petersburg (Urusi)

Polisi nchini Urusi imeyavunja nguvu maandamano dhidi ya rais Vladimir Putin katika mji wa Saint Petersbourg na kuwakamata wapinzani 200 hii leo,akiwemo mwanasiasa wa kiliberali Bortis Nemtsov.”Wameniachia ,najaribu kupigania waandamanaji wengine waachiliwe” amesema Nemtsov,anaepanga pia kutetea wadhifa wa rais katika uchaguzi wa mwezi March mwakani. Nikita Belykh,mkuu wa chama cha SPS-Umoja wa vikosi vya mrengo wa kulia” atakaepigania kiti katika uchaguzi wa bunge december pili ijayo,nae pia amekamatwa.Jana polisi wa Urusi walimkamata bingwa wa zamani wa dama Gari Kasparov.Amehukumiwa kifungo cha siku tano jela kwa makosa ya kuitisha maandamano kinyume na sheria.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com