PARIS: Waziri Mkuu wa zamani Barre amefariki dunia
25 Agosti 2007Matangazo
Aliekuwa waziri mkuu wa Ufaransa,Raymond Barre amefariki katika hospitali ya kijeshi mjini Paris akiwa na miaka 83.
Barre alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 1976 hadi 1981 chini ya Rais Valery Giscard d’Estaing na alikuwa meya wa mji wa Lyon,kati ya mwaka 1995 na 2001.