Obama afurahishwa na maafikiano ya kutosambaa silaha za kinuklia | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 29.05.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Obama afurahishwa na maafikiano ya kutosambaa silaha za kinuklia

Rais Barack Obama amefurahishwa na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa umoja wa mataifa yanayohuzu kuzuwia kusambaa kwa silaha za kinuklia.

default

Rais Barack Obama akitembea kuelekea mahali anapozungumza na waandishi habari katika ikulu ya Marekani White House.

Rais Barack Obama amefurahishwa na makubaliano yaliyoafikiwa katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa, kuhusiana na mkataba wa kuzuia kusambaa kwa silaha za nyuklia. Hata hivyo Obama alipinga vikali, kile alichokitaja ni kuilenga Israel, katika mkutano uliopangwa kufanyika mwaka 2012, na kuyaleta pamoja mataifa yote ya Mashariki ya Kati, ili kuondolea mbali kitisho cha silaha za nyuklia katika Mashariki ya Kati. Mataifa matano yanayomiliki silaha za Nyuklia, na ambayo yametia saini mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha hizo, yalikubaliana kuchukua hatua zaidi kuzuia tishio la silaha za nyuklia duniani. Mataifa hayo yanayoongozwa na Marekani, Urusi, China, Ufaransa na Uingereza- yote yameridhia pendekezo la kupunguza zana zao za nyuklia. Hatua hii sasa inaiwekea mbinyo zaidi Israel, pamoja na India, Pakistan na Korea Kaskazini- mataifa matatu ambayo yamekataa kutia saini mkataba huo wa kusambaa kwa silaha za nyuklia.

 • Tarehe 29.05.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NcW5
 • Tarehe 29.05.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NcW5

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com