NUREMBERG: Kiongozi wa mashtaka wa Nuremberg aanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni ya Siemens | Habari za Ulimwengu | DW | 03.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NUREMBERG: Kiongozi wa mashtaka wa Nuremberg aanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni ya Siemens

Kiongozi wa mashtaka wa Nuremberg ameanzisha uchunguzi kuhusu malipo yaliyotolewa kwa serikali ya rais wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein, na kampuni kubwa ya Kijerumani ya vifaa vya elektroniki ya Siemens.

Maafisa wa upelelezi wanaichunguza kampuni ya Siemens kutambua iwapo ilikiuka sheria za biashara ya kigeni.

Malipo hayo yanasemekana yalitolewa wakati wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa mafuta kwa chakula ulioendeshwa kutoka mwaka alfu moja mia tisa, tisini na sita hadi mwaka alfu mbili na tatu.

Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa wa mwaka alfu mbili na tano uligundua kampuni zaidi ya alfu mbili zilikuwa zimeihonga serikali ya Iraq ili kushirikishwa kwenye mpango wa mafuta kwa chakula.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com