1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Rais wa Iran asema kutoitambia Israel ni kutokana na kunyanyaswa wapalestina

25 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMp

Rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran amesema kuwa nchi hiyo hailitambui taifa la Israel kutokana na uvamizi na ubaguzi wake dhidi ya wapalestina.

Akihutubia jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Columbia jijini New York, kabla ya kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baadaye hii leo, kiongozi huyo wa Iran pia alitetea nishati ya nuklia wanayoirutubisha akisema ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Rais Ahmednejad alihoji ni vipi wapalestina wanabebeshwa mzigo wa mauaji ya wayahudi yaliyofanywa na utawala wa Hitler.

Akijibu swali juu ya haki za mashoga kiongozi huyo wa Iran alisema kuwa jamii hiyo nchini Iran haipo.

Aidha aliishambulia Marekani kwa kumuunga mkono Saddam Hussein wakati wa vita kati ya Iran na Iraq ambapo alisema Saddam alitumia silaha za sumu kuishambulia nchi yake.