NEW YORK:Mjumbe maalum wa UM kutoa taarifa yake leo | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK:Mjumbe maalum wa UM kutoa taarifa yake leo

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa bwana Ibrahim Gambari leo hii atatoa taarifa yake mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu ziara yake ya nchini Myanmar.

Ziara ya mjumbe huyo maalum wa umoja wa mataifa mjini Yangon ililenga kutatua mvutano ulisababishwa na hatua ya autawala wa kijeshi dhidi ya waandamanaji wanao ipinga serikali ya kijeshi.

Balozi wa Ghana katika umoja wa mataifa Lesalie Christian ambae anashikilia uenyekiti wa umoja wa mataifa mwezi huu amearifu kwamba mkutano wa leo utahudhuriwa pia na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon,na wawakilishi kutoka Singapore na Myanmar.

Wakati huo huo mkuu wa kijeshi wa Myanmar jenerali Than Shwe ametanagaza kuwa atakutana na kiongozi anaetetea demokrasia aliye kizuizini bibi Aung San Suu Kyi lakini kwa sharti kwamba ataacha mwito wake wa kuihimiza jamii ya kimataifa kuuwekea vikwazo utawala wa kijeshi wa Myanmar.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com