NEW YORK.Marekani yaitaka China itekeleze maamuzi ya baraza la usalama | Habari za Ulimwengu | DW | 16.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK.Marekani yaitaka China itekeleze maamuzi ya baraza la usalama

Marekani imeitaka China itekeleze azimio la umoja wa mataifa juu ya kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini kufuatia hatua ya nchi hiyo ya kufanya jaribio la silaha za nyuklia.

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa mataifa John Bolton amesema China ni lazima iheshimu azimio 1718 lililopitishwa kwa kauli moja.

Baraza la usalama limeiwekea Korea Kaskazini vikwazo vya biashara ya silaha, bidhaa za anasa na usafiri kwa baadhi ya raia wa Korea Kaskazini.

Marekani imesema azimio la baraza la usalama juu ya kuiwekea vikwazo Korea kaskazini ni mafanikio ya jumuiya ya kimataifa.

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa mataifa John Bolton amesema……

O ton….Leo tunawasilisha ujumbe wenye nguvu na bayana kwa Korea Kaskazini na wote wale wanaokusudia kukiuka mkataba juu ya kuzuia uenezaji wa silaha za nyuklia, kuwa watakabiliwa na hatua kali ikiwa wataendelea kutekeleza mipango ya silaha za maangamizi.

Akitoa hoja kwa niaba ya nchi yake balozi wa Korea Kaskazini kwenye umoja wa mataifa PAK Gil amesema.

O ton…..Hii inaonyesha dhahiri kuwa baraza la usalama limepoteza uadilifu na linaendesha sera za undumakulwili katika kazi yake. Ikiwa arekani itaendelea kuishinikiza Jamuhuri ya watu wa Korea nchi yetu itachukua hatua thabiti na kuzingatia shinikizo hilo kuwa ni tangazo la vita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com