NEW YORK : Utawala wa mpito Ivory Coast kupigiwa kura leo | Habari za Ulimwengu | DW | 01.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK : Utawala wa mpito Ivory Coast kupigiwa kura leo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililogawika hapo jana limeahirisha hadi leo hii uamuzi wa kuidhinisha au la kipindi kengine cha utawala wa mpito kuelekea uchaguzi mpya nchini Ivory Coast.

Rais wa baraza hilo kwa mwezi wa Oktoba ambaye ni mwakilishi wa Japani katika Umoja wa Mataifa Kenzo Oshima amewaambia waandishi wa habari kwamba baraza hilo litakutana tena leo hii kuamuwa iwapo au la kuidhinisha rasimu ya Ufaransa yenye kupendekeza Waziri Mkuu wa Ivory Coast Konan Banny apewe madaraka makubwa zaidi ya utendaji kuongoza serikali ya mpito.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa John Bolton amesema mashauriano yataanza leo hii kuondosha sitafahamu kwa matarajio ya kulipigia kura azimio hilo wakati wa mchana.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com