NEW YORK: Umoja wa Mataifa waoanya kuhusu janga la kiutu nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 04.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Umoja wa Mataifa waoanya kuhusu janga la kiutu nchini Irak

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi-UNHCR-limeonya kuwa janga la kiutu nchini Irak linalosababishwa na mgogoro nchini humo,linazidi kuwa kubwa kwa sababu ya uhaba wa misaada ya kimataifa.Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR,shirika hilo limeshtushwa jinsi jumuiya ya kimataifa inavyojikokota kukabiliana na tatizo la watu waliopoteza makazi yao.Hadi Wairaki milioni 1.6 wamelazimika kuondoka makwao.Wakati huo huo kila mwezi,takriban wakimbizi 100,000 wanawasili Syria na Jordan na hivyo kuwa mzigo mkubwa kwa serikali za nchi hizo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com