NEW YORK : Egeland kuwa mshauri wa Ban juu ya mizozo | Habari za Ulimwengu | DW | 15.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK : Egeland kuwa mshauri wa Ban juu ya mizozo

Mratibu wa zamani wa masuala ya misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Jan Egeland ametangazwa kuwa mshauri mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon juu ya uzuwiyaji wa mizozo.

Raia huyo wa Norway mwenye umri wa miaka 48 atakuwa anamsaidia Ban katika masuala yanaohusiana katika kuzuwiya na kutatuwa mizozo na atasaidia kuimarisha uwezo wa kujenga amani wa Umoja wa Mataifa.

Wakati wa kipindi chake cha miaka mitatu kama mkuu wa masuala ya kibinaadamu wa Umoja wa Mataifa kiongozi huyo wa zamani wa Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Norway na Shirika la Kimataifa la Haki za Binaadamu Amnesty International Egalend aliogoza harakati kubwa kabisa za misaada kufuatia maafa ya gharika la Tsunami la Bahari ya Hindi hapo mwaka 2004.

Egeland pia anajulikana kuwa mtetezi mkali wa masuala ya kibinaadamu likiwemo lile la umwagaji damu katika jimbo la Dafur nchini Sudan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com