New York. Ban Ki –Moon : Uamuzi wa kuwaruhusu wanajeshi wa UN , ishara muhimu kwa Sudan. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

New York. Ban Ki –Moon : Uamuzi wa kuwaruhusu wanajeshi wa UN , ishara muhimu kwa Sudan.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ameueleza uamuzi wa Sudan wa kuwaruhusu wanajeshi 3,000 wa umoja wa mataifa kuingia katika jimbo la Darfur kama ishara muhimu.

Ujumbe huo wa umoja wa mataifa utatoa msaada kwa wanajeshi 7,000 wa umoja wa Afrika katika jimbo hilo.

Kubadilika kwa Sudan kunakuja baada ya miezi kadha ya mbinyo wa kimataifa wa kuwakubali wanajeshi wa umoja wa mataifa wa kulinda amani.

Lakini serikali ya Sudan haijakubali bado kuwekwa kwa jeshi kubwa zaidi la umoja wa Afrika lenye wanajeshi 20,000 ambao wamependekezwa na umoja wa mataifa.

Zaidi ya watu 200,000 wameuwawa katika jimbo la Darfur na zaidi ya milioni mbili wamekimbia makaazi yao tangu mzozo huo uanze mwaka 2003.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com