NEW YORK : Ban aisihi Iraq kusitisha hukumu za kifo | Habari za Ulimwengu | DW | 07.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK : Ban aisihi Iraq kusitisha hukumu za kifo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameisihi sana serikali ya Iraq kusitisha utekelezaji wa hukumu za adhabu ya kifo zijazo kufuatia kunyongwa kwa kingozi wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York baruwa iliotumwa kwa mwakilishi wa kudumu wa Iraq kwenye Umoja wa Mataifa imerudia wito wa Ban wa kutaka serikali ya Iraq kujizuwiya katika utekelezaji wa hukumu za adhabu ya kifo zilizotolewa na Mahkama Kuu ya nchi hiyo.

Saddam alihukumiwa kifo kwa kuhusika na mauaji ya raia hapo mwaka 1982 katika mji wa Washia wa Dujail.Washtakiwa wenzake wawili pia wamehukumiwa kifo lakini hukumu bado haikutekelezwa.

Kwa mujibu wa sheria ya Iraq hukumu hiyo inatakiwa iwe imetekelezwa katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja baada ya kutolewa kwake.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com