1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nepal kupambana na watakaovuruga mbio za mwenge wa olimpik

20 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dl7W

Katmandu:

Nepal imesema itatumia nguvu za kijeshi ikihitajika, kuwazuwia waandamanaji wa Kitibet, kuvuruga shughuli za mbio wa mwenge wa olimpik kwenye mlima Everest. Wanajeshi kadhaa wamewekwa katika maeneo ya mlima huo kabla ya mbio hizo. Uchina mwenye wa michezo ya olimpik ya msimu wa kiangazi mwaka huu bado haijatangaza tarehe ya mbio za mwenge katika mlima huo wenye urefu wa mita 8,850, lakini maafisa wa Nepal wanasema inatarajiwa kuwa kati ya Mei mosi na 10.