NAIROBI:Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa azuru mtaa wa mabanda Nairobi | Habari za Ulimwengu | DW | 31.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI:Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa azuru mtaa wa mabanda Nairobi

Katibu Mkuu wa Umja wa Mataifa Ban Ki-Moon ananyenyekezwa na umasikini aliouona katika mtaa wa mabanda wa Kibera mjini Nairobi nchini Kenya.Kiongozi huyo alizuru mtaa huo hapo jana ulio na makazi chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa Makazi Habitat .

Ziara hiyo inampa nguvu kiongozi huyo kutia juhudi zaidi kushughulikia masuala ya kuimarisha elimu,kupata maji safi,usafi vilevile makazi.Bwana Ki-Moon aliandamana na kiongozi wa mpango huo wa makazi wa Umoja wa mataifa Anna Tibaijuka vilevile waziri wa Elimu wa Kenya George Saitoti.

Kiongozi huyo anatoa wito wa ushirikiano wa karibu kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika AU ili kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo mwaka 2015 hasa katika nyanja za afya,makazi na elimu.

Bwana Ban Ki-Moon anatarajiwa kuelekea nchini Uholanzi ili kufanya mazungumzo na viongozi wan chi hiyo aidha kuzuru mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Uhalifu wa Kivita iliyo The Hague.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com