NABLUS: Mbunge wa Fatah amekamaktwa na Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 29.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NABLUS: Mbunge wa Fatah amekamaktwa na Israel

Wanajeshi wa Israel wamemkamata mbunge wa Kipalestina wa chama cha Fatah cha Rais Mahmoud Abbas.Israel ilikuwa ikimsaka Jamal Tirawi,kwa madai ya kuhusika na harakati za wanamgambo,tangu kuzuka uasi wa Wapalestina katika mwaka 2000. Tirawi,alie msemaji wa Fatah bungeni,alikamatwa pamoja na walinzi wake 4 katika kambi ya wakimbizi ya Balata mjini Nablus.Hii ni mara ya kwanza kwa mwanachama wa Fatah alie mbunge wa Wapalestina kukamatwa na Israel.Sasa Israel imewatia mbaroni zaidi ya wabunge 40 kutoka bunge la Wapalestina lenye viti 132.Wengi waliokamatwa ni wanachama wa Hamas.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com