1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo kati ya Georgia na Urussi kujadiliwa kesho na baraza la usalama

22 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/DlzU

NEW-YORK

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa litakuwa na kikao maalum hapo kesho kujadili juu ya mgogoro kati ya Georgia na Urssi kuhusiana na jimbo lililojitenga la Abkhazia.Mkutano huo unakuja baada ya Georgia kuishutumu Urussi kwa kuishambulia na kuitungua ndege yake moja iliyokuwa angani miongoni mwa ndege zake ambazo hazikuwa na silaha mnamo mwishoni mwa wiki.Kanda wa jeshi la angani la Georgia amesema ndege ya kivita ya Urussi iliishambulia ndege hiyo wakati ilipokuwa ikipaa katika anga ya jimbo lililojitenga la Abkhazia.Hata hivyo hadi sasa serikali ya mjini Moscow imekanusha kuhusika na tukio hilo.Hapo jana viongozi wa nchi hizo mbili walijadiliana kwa njia ya simu kuhusu tukio hilo.Rais wa Georgia Mikheil Saakashvili ameyataja mazungumzo hayo kuwa magumu na kwamba amemtolea mwito Vladmir Putin kukomesha harakati zake za kuunga mkono jimbo hilo lililojitenga na Georgia la Abkhazia.