1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mugabe awataka wafanyabiashara kupunguza bei za bidhaa.

25 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DUFe
Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe katika moja ya mikutano yake ya kampeni nchini humo hivi karibuni. katika eneo la Mubaira Growth Point. kilometa chache kutoka mji mkuu Harare.Picha: picture-alliance/ dpa

Harare.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anatarajiwa leo Jumanne kuamuru maduka kupunguza bei za bidhaa , ikiwa ni siku chache tu kabla nchi hiyo kufanya uchaguzi mkuu, wakati akikabiliwa na madai kuwa anajaribu kununua kura.

Mugabe , ambaye anamatumaini ya kupata kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha sita katika uchaguzi wa siku ya Jumamosi, ameitisha mkutano wa wafanyabishara na wachuuzi ambapo atawataka kupunguza bei katika kiwango kilichokuwapo Februari ama sivyo wanakabiliwa na utaifishaji wa biashara zao.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 84 amekasirishwa na ongezeko la kila siku la bei katika nchi hiyo yenye matatizo makubwa ya ughali wa maisha na kufuta manufaa yaliyopatikana ya ongezeko la mishahara kwa waalimu na wafanyakazi wa serikali.