Mshukiwa wa shambulizi la bomu akamatwa | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mshukiwa wa shambulizi la bomu akamatwa

Maafisa wa polisi nchini Pakistan wamemkamata mwanamume mmoja anayeshukiwa kuhusika kwenye shambulizi la kujitoa muhanga maisha dhidi ya mskikiti mmoja kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Mwanamume huyo alikamatwa katika wilaya ya Charsadda, ambako mshambuliaji wa kujitoa muhanga maisha alijilipua jana miongoni mwa umati wa watu 1,000 waliokuwa wakisali sala ya Idd msikitini.

Maafisa wanashuku wanamgambo wa kiislamu wanaopatikana kwenye mpaka wa Afghanistan walihusika katika shambulizi hilo.

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Pakistan, Aftab Ahmed Khan Sherpao, mfuasi mkubwa wa rais Pervez Musharraf, alikuwa akiongoza sala ya Idd katika msikiti huo wakati shambulizi hilo lilipofanywa. Aliponea chupuchupu lakini watu takriban 80 wakauwawa.

Polisi inasema shambulizi hilo lilimlenga waziri huyo wa zamani kwa kuongoza harakati dhidi ya wanamgambo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com