1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mradi wa Mabomba ya gesi ya Nord Stream 2 Magazetini

Oumilkheir Hamidou
23 Desemba 2019

Mvutano kuhusu mradi wa ujenzi wa mabomba ya gesi ya Urusi, watoto wa wakimbizi waliokwama Ugiriki na taharuki kufuatia onyo la shambulio la kigaidi mjini Berlin,ni miongoni mwa mada magazetini.

https://p.dw.com/p/3VG2V
USA/Deutschland Sanktionen gegen Nord Stream 2
Picha: Reuters/S. Jacobsen

Tunaanzia njia panda inayounganisha Ulaya na Marekani. Ujenzi wa mabomba ya gesi ya Urusi kuelekea Ulaya kwa kuikiuka Ukraine umeikasirisha Marekani iliyoamua kutangaza vikwazo dhidi ya nchi zote zinazohusika na mradi huo. Gazeti la " Passauer Neue Presse" linaukosoa uamuzi wa Marekani na kuandika: "Ujerumani na Ulaya si makoloni ya Marekani. Ukweli huo kila mwanafunzi wa Ujerumani anautambua. Balozi wa Marekani mjini Berlin Richard Grenell , anaonyesha kutopata fursa ya kujifunza hayo aliposomea diplomasia. Nchi za Umoja wa Ulaya zinapokosoa mradi wa  Ujerumani na Urusi kujenga mabomba ya kusafirisha gesi,  hiyo ni shauri yao na ni khiari ya Ujerumani pia kufafanua kwanini ushirikiano pamoja na Urusi haumanishi kwamba sera yake ya nishati inaamuliwa kutoka Moscow. Nchi za Ulaya hazimhitaji Richard Grenell awe mlezi wao na wajerumani hawahitaji muongozo kupitia mbiu ya Donald Trump.

Kadhia ya waakimbizi waliokwama Ugiriki

Kadhia ya kuhuzunisha ya watoto wa wakimbizi waliokwama kaatikia kisiwa cha Ugiriki inaendelea kugonga vichwa vya habari. Gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linaandika:"Sera ya Umoja wa Ulaya kuhusu wakimbizui imefeli. Miaka minne baada ya wimbi kubwa la wakimbizi kutoka mashariki ya kati, mataifa wanachama wa Umoja wa ulaya yangali yanazozana juu ya jinsi ya kusajiliwa  na kugawana wanaoomba kinga ya ukimbizi. Wanasiasa wa ulaya wanazidi kuonya kilichotokea mwaka 2015 kisirudiwe, ingawa kinyume chake ndicho kinachotishia kutokea. Mkuu wa chama cha walinzi wa mazingira Robert Habeck hajakosea alipoonya dhidi ya aibu ya Ulaya. Anazikumbusha nchi za Ulaya jinsi zinavyopenda kuzungumzia  maadili na kumbe wao wenyewe hawayafuati."

Miaka mitatu baada ya shambulio la Breitscheidplatz

Jumamosi iliyopita, takriban, miaka mitatu tangu shambulio la kigaidi lililotokea katika soko la X-Mas katika uwanja wa Breitscheidplatz, hatua kali zilichukuliwa na vikosi vya usalama kusambazwa: Kitisho cha shambulio la kigaidi kwa bahati nzuri hakikuthibitika. Gazeti la "Berliner Morgenpost" linaandika: "Yeyote yule aliyeingiwa na wasi wasi kwasababu ya hatua hizo za pupa za usalama anabidi ajiulize: Wao wangefanya nini?Wangeachia hivi hivi ishara zilizojitokeza katika soko la X-Mas? Wasingefanya hivyo hata kidogo. Hata kama sio kila jaribio lililogunduliwa la mashambulio ya kigaidi lilikuwa nusra lifanyike, tunabidi tushukurie kwamba vikosi vya usalama vimetekeleza jukumu lao ipasavyo. Bora hivyo kuliko vyenginevyo."

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandsprease

Mhariri