MOSCOW:Urusi na Umoja wa Ulaya kujenga ushirikiano mpya asema waziri Steinmeier | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW:Urusi na Umoja wa Ulaya kujenga ushirikiano mpya asema waziri Steinmeier


Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank Walter Steinmeier amesema mjini Moscow , anatumai kuwa Urusi na nchi za Umoja wa UIaya hivi karibuni zitakamilisha mazungumzo juu ya kujenga ushirikiano mpya.

Waziri Steinmeier yupo mjini Moscow kama waziri wa nchi inayoshikilia urais wa tume ya Umoja wa Ulaya kwa sasa.

Mazungumzo juu ya kujenga ushirikiano huyo mpya yalikuwa yaanze mwaka jana lakini lakini yalipingwa na Poland kama ishara ya kulalamika juu ya hatua ya Urusi kupiga marufuku nyama kutoka Poland kuingizwa nchini Urusi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com