1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Waandamana kupinga sera za Putin

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBt9

Mamia ya waandamanaji wameandamana hadi katika uwanja wa St.Petersburg kupinga sera za Rais Vladimir Putin wa Urusi.

Idadi kubwa ya polisi iliwasindikiza waandamanaji hao ambao waliongozwa na bingwa mashuhuri wa zamani wa mchezo wa dama Garry Kasparov.

Maandamano hayo ni mfululizo wa maandamano kadhaa ya wafuasi wa upinzani ambao wanamshutumu Putin kwa kurudisha nyuma maendeleo ya demokrasia kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais nchini humo hapo mwakani.