1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel kushauriana na Rais wa Russia, Vladmir Putin.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZ5

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel anatarajiwa kushauriana na Rais wa Russia, Vladmir Putin, katika mji wa kitalii wa Sochi nchini Russia.

Hiyo ndio ziara ya kwanza ya Kansela Angela Merkel nchini humo tangu Ujerumani ilipokamata urais wa Umoja wa Ulaya na pia kundi la mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8.

Uhusiano kati ya Russia na Umoja wa Ulaya umezorota tangu majuma mawili yaliyopita, wakati Russia ilipokatiza huduma ya mafuta kupitia bomba kuu kuelekea mataifa ya Ulaya.

Kansela huyo wa Ujerumani anatarajiwa kuisisitizia Russia kuwa mtoa mafuta wa kutegemewa.

Viongozi hao wawili pia wanatarajiwa kujadiliana kuhusu juhudi za kufufua mashauriano ya amani ya Mashariki ya Kati.