MOGADISCHU:Magari yatiwa moto na maduka kuporwa katika mji mkuu wa Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISCHU:Magari yatiwa moto na maduka kuporwa katika mji mkuu wa Somalia

Mogadischu:

Vikosi vya Ethiopia na vile vya serikali ya mpito ya Somalia vinaendelea kuwasaka wanaharakati wa kiislam waliojificha katika msitu wa Badade karibu na mpaka wa Somalia na Kenya.”Wanaharakati wa kiislam wamejificha msituni lakini tutawaandamana mpaka mwisho” amesema kamanda Abdulrazak Afgebub akiwa mjini Kismayu.Marekani imejiunga pia na opereshini hizo kwa kutuma manuary zake katika fukwe za Somalia ili kuzuwia wanaharakati wa kiislam wasitoroke kupitia baharini.Wakati huo huo machafuko yameripuka hii leo mjini Mogadischu kati ya waandamanaji wanaopinga kujiingiza kati Ethiopia na vikosi vya Somalia.Mashahidi wanasema waandamanaji wametia moto mipira ya magari na kuwavurumishia mawe wanajeshi wa kisomali.Maduka pia yamevunjwa-mashahidi hao wameendelea kusema.Wakati huo huo serikali ya Somalia imeakhirisha mpango wa kuwapokonya silaha kwa nguvu raia.Jana Marekani na Umoja wa ulaya walitangaza utayarifu wao wa kugharimia shughuli za kulinda amani za vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia.Uganda imesema iko tayari kuchangia wanajeshi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com