Mkutano wa uhaianwai mjini Bonn | Magazetini | DW | 29.05.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Mkutano wa uhaianwai mjini Bonn

Mchango wa Ujerumani kuengezeka mara dufu

default

Picha za uhaianwai


Mjadala wa bunge kuhusu dhana za ushirikiano kati ya mwenyekiti wa chama cha mrengo wa shoto Die Linke Gregor Gysi na idara ya zamani ya upelelezi katika Ujerumani mashariki ya zamani-Stasi,kuchaguliwa waziri mkuu wa jimbo la Sachsen Tillich na mkutano wa Umoja wa mataifa kuhusu UHAIANWAI mjini Bonn.


Tuanze basi na mkutano wa kuhifadhiwa UHAIANWAI,ambapo gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linamulika zaidi azma ya serikali kuu ya Ujerumani ya kutenga kitita kikubwa cha fedha kwaajili ya kuhifadhiwa misitu ya joto.Gazeti linaendelea kuandika:"Lazma ni milioni mia kadhaa hizo zitakazotolewa ili angalao kudhihirisha umuhimu ulioko kwa sasa.Kansela ameahidi mamilioni ya fedha kama ushahidi bayana wa jukumu la Ujerumani kuelekea mazingira.Ikiwa katika kipindi cha siku mbili zijazo mataifa tajiri kiviwanda yatajadiliana usiku na mchana kuhusu hifadhi jumla ya uhaianwai,kuna watakaotaka kujua bila ya shaka,hatua za aina gani mataifa hayo yanapanga kupitisha?Mkutano wa Bonn unajadiliana juu ya namna ya kuihifadhi hazina ambayo ni tunu na isiyogawika ya dunia yetu hii,na jinsi kila mmoja anavyopaswa kuwajibika ipasavyo ili kuinusuru hazina hiyo.Kwa hivyo mamilioni yaliyoahidiwa na Merkel yanastahiki.Lakini matarajio ya mkutano huo ni duni sawa na hali inavyokua katika mikutano mengine kama hii."


Gazeti la DIE TAGESZEITUNG linasifu na kuandika:


"Hakuna aliyetajaria kwamba yuro nusu bilioni zitakua zikimiminika kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2013.Serikali kuu ya Ujerumani inafakhari pia kuhusu ahadi za fedha zilizotolewa.Waziri wa mazingira Sigmar Gabriel anaeongoza mkutano huo anafanya kila liwezekanalo ili mkutano huo ufanikiwe.Kansela Merkel amebainisha,sawa na wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa,amepania kweli kweli kuchangia katika kuhifadhiwa uhaianwai.


Hayo ni maoni ya TAZ,nalo gazeti la DIE WELT linaandika:


"Ukipiga hesabu utaona kwamba tangazo la Merkel linahusu kuongezeka mara dufu mchango wa Ujerumani katika sekta ya ulinzi wa mazingira.Hicho ni kilele na hakuna anaweza kubisha kama kama Merkel si kipenzi cha mazingira.Yadhihirika kana kwamba ana ratiba maalum upande huo.Baada ya mkutano kuhusu mageuzi ya hali ya hewa,unafuatia kuu wa uhaianwai."


FRANKFURTER RUNDSCHAU lina maoni tofauti kabisa kuhusu kile kilichosemwa na kansela Merkel,na linaandika:


"Mabilioni kwaajili ya mazingira tuu yaliyoingia hatarini.Na maneno matamu matamu.Ungetamani kujiunga na wale waliokua wakishangiria katika mkutano wa uhaianwai mjini Bonn,kama hakukua na walakin.Hali kama hii imeshawahi kutokea.Mwaka mmoja baada ya Heiligendamm,hakuna ahadi yoyote ya malkia wa hali ya hewa iliyotekelezwa.Sifa yake kama mlinzi wa mazingira imechujuka.Aling'ara alipoahidi kuchangia kuhifadhi hali ya hewa.Nchini mwake mwenyewe ameshindwa hata kutia njiani kodi ya wenye magari ambayo ingesaidia kuhifadhi hali ya hewa.Yuro tatu tuu za ziada kwa mwezi kwa kila mwenbye kumiliki gari.Wanahisi ni ghali mno kuhifadhi dunia yetu.Kuna zaidi ya hayo?
 • Tarehe 29.05.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E8He
 • Tarehe 29.05.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E8He
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com