Mkutano wa kwanza kati ya umoja wa Ulaya na mataifa ya Asia ya kati wafanyika leo. | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.03.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa kwanza kati ya umoja wa Ulaya na mataifa ya Asia ya kati wafanyika leo.

Leo Jumatano mkutano unafanyika katika mji mkuu wa Kazakstan kati ya ujumbe wa umoja wa Ulaya ukiongozwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na viongozi kadha wa mataifa ya Asia ya kati. Mkutano huo ni wa kwanza kati ya umoja wa Ulaya na mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa matano ya iliyokuwa Urusi ya zamani katika eneo la Asia ya kati. Taarifa na Thomas Nehls.

Lengo la mkutano huo ni kuunda mkakati mpya wa eneo hilo la Asia ya kati pamoja na umoja wa Ulaya.Mpango huo kwa hiyo unatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa umoja wa Ulaya kabla ya muda wa urais wa Ujerumani katika umoja wa Ulaya kumalizika katika majira ya joto mwaka huu.Steinmeier ambaye amezitembelea nchi hizo Novemba mwaka jana , anaongozana katika ziara hiyo na kamishna wa masuala ya mambo ya kigeni katika umoja wa Ulaya Benita Ferrero-Waldner na mjumbe maalum wa umoja huo katika mataifa ya Asia ya kati Pierre Morel. Wanaoshiriki katika mkutano huo ni pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kazakhistan , Kirgistan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbenistan.

Ujumbe huo wa umoja wa Ulaya unakabiliwa na mtihani mkubwa hata hivyo mbele yao. Uzbekistan kutokana na uchunguzi juu ya mauaji yaliyofanywa na serikali dhidi ya waandamanaji miaka karibu miwili iliyopita , ilipaswa kukubali vikwazo vilivyowekwa na umoja wa Ulaya , ambapo kushiriki kwake kunaweza kukaiondolea masharti iliyowekewa.

Tunazungumzia juu ya iwapo shirika la kimataifa la msalaba mwekundu linaweza kuingia tena katika jela za Uzbekistan. Tunazungumzia juu ya iwapo sisi pamoja na Uzbekistan

tuwemo katika utaratibu, ama tuwe na majadiliano ya pamoja juu ya haki za binadamu, kama itawezekana kuwa na mustakbali tutakaokubaliana.

Kwa upande wa kiuchumi umoja wa Ulaya unataka kupata nafasi juu ya nishati iliyopo katika mataifa hayo ya Asia ya kati. Asilimia tano ya hifadhi yote ya mafuta na gesi ya ardhini duniani inapatikana katika ardhi ya eneo hilo, hususan nchini Kazakstan, ambayo ina ukubwa wa eneo lote la Ulaya magharibi , lakini inawakaazi wapatao milioni 15 tu. Hapa upungufu unaoonekana wazi. Akielezea juu ya zingatio linalohitajika katika uhusiano huo Steimeier amesisitiza kwamba,

tunalazimika hapa kutokuonekana kuchukua tahadhari kubwa. Tunafahamu wazi kuwa msimamo takriban wa viwango vya umoja wa Ulaya uko kiasi gani na unaathari gani. Tofauti ni kwamba tumejitayarisha vya kutosha.

Lakini hali hii ya kujitayarisha inaweza kupungua, iwapo nchi hizo hazitaimarishwa, na jirani yao mkubwa China itagonga hodi katika mataifa hayo na kuyapa fedha nyingi za mikopo, bila ya kuwekewa masharti yoyote yale.

 • Tarehe 28.03.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHHL
 • Tarehe 28.03.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHHL
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com