Mkataba wa Geneva unafanyakazi kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu. | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.06.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkataba wa Geneva unafanyakazi kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu.

Picha ya mtoto akiwa amekaa katika maba ki ya mlipuko wa bomu nchini Azeibajan , mama nchini Yemen akipokea ujumbe kutoka kwa mtoto wake kutoka Guantanamo Bay, wagonjwa waliojeruhiwa katika vita nchini Pakistan, hizi ni picha zinazoonyesha athari za mapambano ya kivita katika nchi kadha kati ya mwaka 1971 na 2006 zikiwa sehemu ya maonesho ya picha yaliyopewa jina la `Utu katikati ya mizozo`, ambayo yamefunguliwa katika makumbusho ya taifa ya Australia mjini Canberra, katika kuadhimisha mwaka wa 30 wa kuongezwa kwa vipengee moja na mbili vya mkataba wa Geneva.

Mkataba huo unabaki kuwa muhimu katika kuwalinda raia katika maeneo ya mizozo na kurekebisha zaidi jinsi ya uendeshaji wa vita. Picha hizi zinaonyesha madhila ya kiutu katika mizozo ya kivita. Pia zinatukumbusha kuwa, hata wakati wa vita, hii ndio mipaka, amesema Pauline Wall kutoka katika shirika la kimataifa la msalaba mwekundu, ICRC.

Iwapo vita vilikuwa vigumu kueleweka katika mwaka 1977, imekuwa vigumu zaidi katika mwaka 2007. Mapambano ya silaha yamekuwa hivi sasa aghalabu kati ya taifa na taifa , lakini mara nyingi ni suala la ndani, linalowahusisha makundi tofauti. Raia mara nyingi ndio wanaoangukia kuwa wahanga wa vita, wakiwakilisha karibu asilimia 90 ya wahanga katika mizozo inayotokea hivi sasa. Pamoja na kujikuta katika mapigano na kuwa kama kile kinachojulikana kama uharibifu ziada, lakini mara nyingi wanalengwa maksudi, kama inavyotokea nchini Iraq na Afghanistan.

Mara nyingi wale wanaobeba silaha hawaheshimu sheria za kimataifa za kiutu. Picha hizi zilichochukuliwa na wapigapicha wataalamu, pamoja na wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu , zinaleta uhalisi wa unyama ambao mapambano ya silaha yanaendelea kuathiri raia.

Raia wanakumbana na matumizi ya nguvu, kupoteza nyumba zao pamoja na kupotezana wanafamilia baada ya kukimbia huku na huko kusalimisha maisha yao, na wanakosa chakula, maji na huduma za utatibabu, anasema Jean-Luc Metzker, mkuu wa ujumbe wa kimkoa wa shirika la msalaba mwekundu katika eneo la Pacific.

Nyongeza ya mwaka 1977 katika mkataba huo , ambayo inasema kuwa mkataba wa mwaka 1949 wa Geneva , umekuwapo kutokana na kubadilika kwa sura ya mapambano, hususan kuzuka kwa vita vya msituni pamoja na maendeleo ya kiufundi katika teknolojia ya silaha. Kupanuka kwa uwanja wa vita hadi kwa raia kunaleta hatari kubwa , na mkataba umeimarisha ulinzi wa wahanga wa mapambano hayo ya silaha. Nyongeza ya kipengee nambari mbili kwa mara ya kwanza imeongeza ulinzi kwa raia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wakati mkataba huo unakubalika duniani kote, dunia lakini imejaa mifano kadha ya sheria kuendewa kinyume katika mizozo ya leo iwe ni Iraq, Afghanistan , Sudan ama Colombia ama Rwanda na katika maeneo ya Balkan. Kampeni za kigaidi dhidi ya raia na vitendo vya ubakaji, uandikishaji wa wapiganaji watoto , kuwalazimisha watu kukimbia makaazi yao, hayo yote yamekuwa ni mazoea katika wakati huu.

 • Tarehe 08.06.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHCy
 • Tarehe 08.06.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHCy

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com