MINNEAPOLIS : Bush azuru eneo la ajali ya daraja | Habari za Ulimwengu | DW | 05.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MINNEAPOLIS : Bush azuru eneo la ajali ya daraja

Rais George W. Bush wa Marekani ametembelea daraja la barabara kuu ambalo limeanguka kwenye Mto Misisipi Jumaatano iliopita.

Baada ya kuliangalia eneo hilo kwa safari ya helikopta Bush amekutana na wahanga na wafanyakazi wa uokozi na kuahidi kulijenga upya kwa haraka daraja hilo.

Takriban watu watano wameuwawa na wengine madarzeni kujeruhiwa katika maafa hayo ambayo yametokea wakati wa sasa za harakati za jioni.Polisi hapo jana wamesema watu wanane bado hawajulikani walipo na wazamia mbizi wanaendelea kuwatafuta wahanga.

Sababu ya ajali hiyo bado haijulikana na uchunguzi unaendelea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com