Michezo:Finali ya kombe la dunia | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 14.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Michezo:Finali ya kombe la dunia

AC Milan na Boca juniors zacheza finali ya kesho uwanjani Yokohama,Japan kuania kombe la dunia.

Duru ya kwanza ya kombe la challenge Cup-kanda ya Afrika mashariki na kati takriban imemalizika na mpambano wa jioni ya leo ni kama ada tu-kwani timu zinazoingia robo-finali itayoanza jumatatu mjini Dar-es-salaam zajulikana.

Iliowasangaza mashabiki hadi sasa, ni zanzibar Heroes waliofungua dimba kwa suluhu na Sudan 2:2-timu pekee itakayocheza mwezi ujao huko Ghana kombe la Afrika la mataifa.Baadae zanzibar ikaizaba Ethiopia mabao 3:1.

Kesho ni finali ya kombe la klabu bingwa duniani kati ya mabingwa wa ulaya Ac Milan na mabingwa wa Amerika kusini -Boca Junior ya Argentina.Je, Kaka wa Brazil na Seedorf wa Holland watawika wakiichezea Milan?

Katika Bundesliga,Bayern Munich yabidi leo kucheza na Berlin bila kipa na nahodha wao Oliver Khan-kisa ni nini ?

Tuanze na kombe la challenge cup-kombe la Afrika mashariki na kati linaloaniwa kuanzia sasa Dar-es-salaam .Timu zitakazoshiriki katika robo-finali ya kombe hilo zajulikana na ya kusangaza kabisa imekuwa Zanzibar Heroes. Zanzibar ilitoka suluhu na mabingwa watetezi Sudan 2:2 na kuichapa Ethiopia 3:1 .Zanzibar ikaifuata Uganda ,tanzania-bara,Ruanda na Burundi katika robo-finali inayoanza jumatatu ijayo.

Kesho asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano uwanjani Yokohama Stadium, uwanja ule ule Brazil na Ujerumani ziliumana 2002 kuania finali ya kombe la dunia.

Kesho lakini ni finali ya kombe la dunia la klabu bingwa kati ya mabingwa wa Ulaya AC Milan ya Itali na mabingwa Amerika kusini boca Juniors wa Argentina.

Mabingwa wa Afrika Etoile du Sahel ya Tunisia walizabwa bao 1:0 na Boca katika nusu-finali wakati Milan ilitimua nje Urawa United ya japan pia kwa bao 1.

Na ni atamfumania mwenziwe kesho na kutoroka na kombe ni vigumu kuagua.Waargentina lakini watapaswa kukaa macho na kumchunga Kaka wa Brazil asiwaadhibu.

Kocha wa Milan Carlo Ancelotti amebashiri zahama ya kesho itakua ya mpapurano mkubwa na kutoana jasho .“Nadhani itakua mechi ya ngware sana“ alisema Ancelotri.Milan ina uchu wa kulipiza kesho kisasi kwa Boca kwa kupokonywa kombe la Toyota , 2003.Kocha Ancelotti amefunua kawa aliposema mbrazil Kaka aliemchezesha juzi seedorf wa holland kutia bao lililoipiga kumbo Urawa united ya japan ,ataongoza kesho mashambulio ya Milan.

Bundesliga –ligi ya Ujerumani inarudi uwanjani leo alaasiri kwa viongozi wa Ligi-Bayern munich wakicheza na Hertha Berlin bila ya nahodha na kipa wao Oliver Kahn.Kan amefungiwa kucheza leo na kocha wake Ottmar Hitzfeld na amepigwa faini ya kitita cha dala 37.500 kwa kuwakosoa hadharni mastadi 2 wa bayern Munich:Luca toni wa Itali na Riberry wa Ufaransa.

Ikiwa leo Munich itateleza mbele ya Berlin huko Berlin, na Bremen ikitamba ,itapoteza usukani wa ligi alao kwa m waka huu.

Mapambano mengine leo ya Bundesliga: Schalke yacehza na Nuremberg.Brem,en iko nyumbani ikiumana na Leverkusen.Armenia BNielefeld inawakaribisha nyumbani mabingwa Stuttgart wakati Wolfsburg wana miadi na Borussia Dortmund.Karlsruhe inahetimisha leo kwa kupamabana na Hamburg.

Katika Premier League,Arsenal na Liverpool –timu 2 zilizopoteza rekodi zao za kutoshindwa hasta mara 1 wiki iliopita ,zina miadi moja na Chelsea na nyengine na manchester united.Chelsea ikitamba mbele ya Arsenal kesho itakuwa pointi sawa nayo kileleni.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com