MIAMI: Raia wa Kimarekani akutikana na hatia ya ugaidi
17 Agosti 2007Matangazo
Mmarekani alieshtakiwa ugaidi na kuzuiliwa kama „mpiganaji adui“ kwa zaidi ya miaka mitatu katika jela ya kijeshi,amekutikana na hatia nchini Marekani.
Jose Padilla aliesilimu,anakabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela kwa maisha.Amekutikana na makosa ya kufanya njama ya kuuwa,kuteka nyara na kujeruhi watu nchi za ngámbo pamoja na kusaidia ugaidi.Jaji amepanga kumhukumu Padilla tarehe 5 Desemba.