Mbali nakuwa kumiliki silaha nchi Yemen limekuwa suala la Kiutamaduni lakini ukweli ni uvunjWaji wa sheria. | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mbali nakuwa kumiliki silaha nchi Yemen limekuwa suala la Kiutamaduni lakini ukweli ni uvunjWaji wa sheria.

Utamaduni wa kumiliki silaha nchini Yemen umekuwa ukikiuka sheria kutokana na upungufu wa mahakimu mbali na juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali za kuzuia matumizi ya silaha.

default

Mtoto aliyeshikilia buduki ya uongo.

Wanasiasa nchini Yemen wanasema Kitendo cha kubeba silaha kimekuwa kikikingiwa kifua zaidi katika Taifa hilo la Kiarabu ambako mkazi mmoja kutoka kabila lililoko Mashariki Kaskazini mwa jimbo la Marib alitengwa na watu wa ukoo wake pale alipoamua kuitupa bunduki yake.

Daktari mwenye umri wa miaka 36, ambaye alipenda kutajwa jina lake moja tu la kwanza, Ahmad, anasema baada ya kuhitimu elimu yake ya juu katika chuo kikuu nchini Iraq alitambua kuwa elimu yake ndiyo kitu cha msingi na silaha yake ya kweli, wala siyo silaha ya bunguki utamaduni ambao ameurithi kutoka kwa watu wa kabila lake.

Ahmad ameliambia Shirika la habari la Ufaransa kuwa hata hivyo uamzi wake huo, haukukubalika kwa familia yake na hata kwa watu wengine wa kabila lake na hivyo ikamubidi ahame jimbo la Marib na kwenda kuishi katika mji wa Taiz ulioko Kusini mwa mji wa kibiashara wa Sanaa ili akaishi huru na kuachana na utamaduni wa matumizi ya bunduki.

Yemen inakadiliwa kuwa na bunduki milioni sitini ambazo zinamilikiwa na watu binafsi ambapo kila raia watatu kati yao mmoja anakuwa nayo.

kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Rashad al-Alimi, kuna kesi zipatazo ishirini na nne elfu mia sita ishirini na tatu za watu ambao wamehusika katika mashambulizi ya silaha katika kipindi cha mwaka 2004 na 2006.

Katika taarifa hiyo Rashid al-Alimi anasema ni asilimia themanini na saba ya kesi ambazo zimesharipotiwa katika kipidi chote ambazo zilisababisha vifo vya watu Ishirini na tatu elfu mia tano sabini na saba.

Aidha waziri huyo wa mambo ya ndani wa Yemen amesema kwamba hali hiyo ni moja ya changamoto inayoikabili wizara ya ulinzi ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na tishio la ugaidi na kulinda mipaka yake.

Ni mwaka jana tu Serikali ya Yemen ilitangaza sheria mpya ya kupambana na matumizi ya silaha kwa kuwazuia watu kutumia na kumiliki silaha hizo katika mji wa Sanaa na miji mingine mikubwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Serikali ya nchi hiyo ni bunduki elfu tisini zimeshapokonywa kutoka kwa raia wa kawaida.

Sheikh Hamid Abdullah al-Ahmar, mtoto wa aliyekuwa spika wa Bunge Sheikh Abdullah Al-Ahmar na kaka yake Hussein, wameliambia Shirika la habari la AFP, kitendo cha kubeba silaha kilikuwa ni cha heshima na utambulisho kwa mwanamume wa Yemen na wala haikuwa starehe.

Anasema hata hivyo hakuna haja ya raia wa Yemen kuendelea kuang'ang'ania kumili silaha wakati jirani zao wa ghuba ambao wanatoka kabila moja na wao wameshazisalimisha silaha zao.

Hata hivyo Daktari Ahmad, anasema upungufu uliopo katika sheria na udhaifu katika Wizara ya ulinzi uliofanywa na Serikali wa kutowatafuta watu ambao wamekuwa wakiendesha mauaji ni moja ya sababu kubwa zinazochangia kuendelea kwa mauaji hayo.

 • Tarehe 02.04.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DZRQ
 • Tarehe 02.04.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DZRQ
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com