1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa fedha wa nchi tajiri wakutana Tokio

9 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4tT

Tokio:

Mawaziri wa fedha na wakuu wa benki kutoka mataifa sabaa tajiri kiviwanda-G7 wanakutana mjini Tokyo-Japan kwa mashauriano kuhusu madhara yanayoweza kutokana na mizozo inayozikumba benki wakazi huu tulio nao.Waziri wa fedha wa Japan FUKUSHIRO NUKAGA amesema,wanataka kwanza kutathmini hali jumla namna ilivyo na baadae kutuma risala ya nguvu kwa lengo la kutuliza hali ya mambo katika masoko na nguzo nyengine za kiuchumi ulimwenguni.Waziri wa fedha wa serikali kuu ya Ujerumani Peer Steinbrück anasisitiza haja ya kuimarishwa hali ya uwazi katika masoko ya fedha.Mbali na mataifa saba tajiri kiviwanda-Marekani,Japan,Ujerumani,Canada,Uingereza,Ufaransa na Italy,wajumbe wa Urusi,China na Indonesia nao pia wanahudhuria mkutano huo wa Tokyo.