1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema Ukraine itajiunga na NATO

Josephat Charo
4 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Ukraine itajiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO wakati muungano huo wa kijeshi ukiadhimisha miaka 75 tangu kuasisiwa kwake.

https://p.dw.com/p/4eRFc
Waziri wa Mambo wa Nje wa Marekani, Antony Blinken.
Waziri wa Mambo wa Nje wa Marekani, Antony Blinken.Picha: Saul Loeb/AP/picture alliance

Akizungumza katika makao makuu ya NATO mjini Brussels akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, Blinken amesema lengo lao kwenye mkutano wa kilele wa mjini Brussels ni kusaidia kujenga daraja kuelekea uanachama huo na kuisafisha njia Ukraine isonge mbele.

Soma zaidi: Mawaziri wa NATO wakutana na kuahidi mshikamano na Ukraine

Blinken pia amesema ni muhimu kwamba bunge la Marekani lisonge mbele na ombi la nyongeza ya bajeti ambalo Rais Joe Biden wa Marekani aliliwasilisha kwa msaada zaidi kwa Ukraine.

Kwa upande wake,Kuleba amesema NATO imekubali kutambua na kutafuta mifumo ya ulinzi wa anga katika maghala yao ya silaha na kuzipeleka Ukraine ili kuiwezesha kujilinda.