Marekani kuunda Bodi ya Amani kwa ajili ya Gaza
16 Januari 2026
Hatua hii inanuia kuunda kikundi kipya kinachoitwa Bodi ya Amani, na Rais wa wa Marekani Donald Trump anataka kuongoza mwenyewe bodi hii. Licha ya mpango huu kukosolewa na watu wengi,bado baadhi ya nchi za Ulaya zinataka kujiunga.
Bodi hii ya amani inatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya mchakato wa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina, kama ilivyaoainishwa katika mkakati wenye vipenegere 20 vya amani unaoongozwa na Rais Donald Trump.
Bodi hii inatarajiwa kutatua changamoto nyingi za kiusalama katika ukanda wa Gazakwa kuzingatia mambo matatpia kusimamia serikali ya muda ya Palestina ambayo hata hivyo haitakuwa na chama cha kisiasa.
Trump ameshatangaza kwamba atasimamia mwenyewe bodi hiyo na kufuatilia utendaji kazi wake. Mpango huu wa kuleta amani katika eneo la Gaza utakuwa na wanachama 15 na tayari umeshapitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Usalama.
Hata hivyo wakosoaji wa mpango huu wanasema hauna uhakika na una mapungufu mengi kwa sababu unawanyima haki na mamlaka wapalestina kuhusu mustakabali wao. Pia wanasema mpango huu unaipendelea Israel kwa kuipa mamlaka katika ardhi ya wapalestina, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za kimataifa kuhusu mamlaka ya mataifa.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemteua Nickolay Mladenov, mwanadiplomasia kutoka Bulgaria, kuwa kiongozi wa Bodi hii ya Amani. Mladenov hapo awali alifanya kazi katika Umoja wa Mataifa kama mkurugenzi wa juhudi za amani katika eneo la Mashariki ya Kati na anajulikana katika pande mbili yaani viongozi wa Israel na Palestina. Hata hivyo inatarajiwa kwamba baadaye watatangazwa wanachama wengine wa bodi hiyo.
Trump atarajiwa kutangaza majina ya wanachama kwenye bodi ya amani kwa Gaza
Taarifa zinasema kwamba Rais Trump anaweza kutangaza majina mapya ya wanachama kabla ya mkutano wa kwanza wa bodi hiyo, katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaotarajiwa kufanyika huko Davos nchini Uswisi. Nchi zinazotarajiwa kualikwa ni pamoja na Saudi Arabia, Qatar, Misri, Uturuki, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, na Italia.
Baadhi ya ripoti za wadadisi zinasema, huenda ya serikali ya Trump inataka kuitumia bodi hii ya amani ya Gaza kwa ajili ya kufanya kazi katika kutatua mizozo mingine duniani hususan mzozo wa Urusi na Ukraine, na pengine inahisiwa kuwa bodi hii inaweza kuchukua baadhi ya mamlaka ya Baraza la Usalama Umoja wa mMtaifa na hatimaye kuchukua nafasi ya shughuli za baraza hilo.
Wazo hili linazifanya baadhi ya nchi kuwa na wasiwasi kwa sababu bodi hii itafanya kazi nje ya mfumo wa kawaida wa utendaji kazi wa baraza hilo la Umoja wa Mataifa.
Wanasayansi wengi wa Ulaya wanataka kujiunga na Bodi hii ya Amani, lakini wengi wanasema watashiriki tu ikiwa kutakuwa na sheria za wazi na ulinzi wa masharti yake. Wanasema kwamba Ulaya inapaswa kuwa makini ili isione kana kwamba inaunga mkono mpango usio sawa.
Kanda ya Mashariki ya Kati ilitumbukia kwenye machafuko makubwa kufuatia Mzozo wa Israel na Hamas.