Maoni ya wahariri juu ya Syria na Ugiriki | Magazetini | DW | 27.08.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya Syria na Ugiriki

Katika maoni yao wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanauzingatia mgogoro wa Syria na kampeni za uchaguzi nchini Ujerumani kuhusiana na mgogro wa madeni wa Ugiriki.

Rais Barack Obama wa Marekani

Rais Barack Obama wa Marekani

Gazeti la "Nürnberger" linatoa maoni juu ya Rais Obama.

Mhariri wa gazeti hilo anasema kwa mara nyingine Obama anayalipa kwa makosa aliyoyafanya katika kuupuuza umuhimu wa sera za nje. Na kosa kubwa sana ni kumpuuza Rais Wladimir Putin wa Urusi. Mhariri wa "Nürnberger" anasema Putin anastahiki kuwapo katika kila meza ya mazungumzo linapohusu suala la Syria.

Gesi ya sumu:

Gazeti la "Frankfurter Allgemeine" pia linatoa maoni juu ya Rais Obama kuhusiana na vita vya nchini Syria. Mhahiri huyo anasema sasa Rais Obama amesimama mkabala na suala ambalo halakuli hali angelipendelea kuliepuka.

Jee achukue hatua za kijeshi dhidi ya Syria bila ya ridhaa ya Umoja wa Mataifa na hivyo kuingia katika mkondo wa dafrao na Urusi na China? Sababu za Marekani kutojiingiza kijeshi nchini Syria mpaka sasa zinafahamika.Lakini sasa Rais Obama anapaswa kujitokeza wazi, la sivyo kauli aliyoitoa haitakuwa na maana, kwamba atachukua hatua ikiwa uwatala wa Assad utaivuka mipaka fulani.

Mhariri wa gazeti la "Münchner Merkur" anauzungumzia utatanishi juu ya silaha za sumu. Jee zimetumiwa na nani? Mhariri huyo anaeleza kwamba dunia inatumai kwamba busara itatangulia mbele ya hoja ya vita miongoni mwa mataifa makubwa ili isije ikajirudia hali kama ile iliyosababisha vita vya Irak mnamo mwaka wa 2003. Ikiwa itathibitika bila ya kuwapo shaka hata kidogo ,kwamba Assad ametumia gesi ya sumu kuwaangamiza watu wasiokuwa na hatia, basi awajibishwe. Hatahivyo yapasa kuzingatia kwamba mustakabal wa eneo lote la Mashariki ya Kati utakuwamo hatarini.

Tahadhari kabla ya hatari:
Gazeti la "Augsburger Allgemeine" linatahadharisha juu ya hatari ya kuchukua hatua kwa kuzitumia tuhuma tu. Mhariri wa gazeti hilo anasema njia hiyo haitakuwa ya busara.

Ugiriki yahitaji msaada mwingine:

Gazeti la "Mannheimer Morgen"linaizungumzia kampeni za uchaguzi mkuu nchini Ujerumani,ambapo suala la msaada kwa Ugiriki limo katika vinywa vya wanasiasa baada ya Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble kusema Ugiriki itahitaji msaada mwingine.

Mhariri huyo anaeleza kwamba Kwa kawaida masuala yasiyovutia hayaguswi wakati wa kampeni za uchaguzi lakini kauli ya Waziri Schäuble ni sahihi.

Na mhariri wa gazeti la "Ludwigsburger Kreiszeitung" anasema alichokifanya Waziri Schäuble ni kusema ukweli. Ugiriki ilipata msaada wa kwanza, ukafuatia wa pili na sasa utafuatia mwingine. Wananchi wa Ujerumani sasa wanakijua kinachowasubiri.

Mwandishi:Mtullya Abdu. Dueutsche Zeitungen.

Mhariri:Yusuf Saumu