Maelfu ya watu wahudhuria tamasha la muziki ″46664″ | Habari za Ulimwengu | DW | 01.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Maelfu ya watu wahudhuria tamasha la muziki "46664"

Maelfu ya watu wamemiminika katika mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini kuhudhuria tamasha la muziki lililozinduliwa na rais wa zamani Nelson Mandela.Hii ni mara ya tano kwa wanamuziki wa kimataifa kujitolea kushiriki katika tamasha linalojulikana kwa namba 46664. Hiyo ilikuwa namba ya Mandela alipokuwa jela.

Kiasi ya watu 50,000 wanatazamiwa kuhudhuria tamasha la wanamuziki 30 wa Afrika Kusini na kutoka nchi za kigeni.Mandela amesema,dunia nzima inapaswa kusimama pamoja na kueleza tishio la UKIMWI na hatua zichukuliwe kutokomeza ugonjwa huo.Afrika Kusini ni nchi yenye idadi kubwa kabisa ya watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,kutoka umma wa milioni 48 nchini Afrika Kusini,kiasi ya milioni 5.5 wameambukizwa virusi hivyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com