LUSAKA:Rais Mwanawasa amwonya kiongozi wa upinzani dhidi ya kuunda serikali sambamba | Habari za Ulimwengu | DW | 10.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUSAKA:Rais Mwanawasa amwonya kiongozi wa upinzani dhidi ya kuunda serikali sambamba

Rais Mwanawasa wa Zambia amemwonya kiongozi wa upinzani nchini humo Bwana Michael Sata kuwa anaweza kufunguliwa mashtaka ya uhaini ikiwa ataendesha serikali sambamba katika maeneo kama Lusaka na katika jimbo la Copperbelt ambapo mabaraza ya upinzani yalichaguliwa.

Bwana Sata amedai kuwa udanganyifu ulifanyika na kwamba ushindi wake uliibiwa, katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita nchini Zambia.

Kiongozi huyo wa upinzani aliongoza katika hatua za mwanzo za uchaguzi na hasa katika miji mikubwa lakini hakufua dafu katika sehemu za mashambani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com