LUANDA: Mafuriko yakumba maeneo ya kusini mwa Afrika. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUANDA: Mafuriko yakumba maeneo ya kusini mwa Afrika.

Mafuriko yamekumba maeneo makubwa ya Angola, Zambia na Msumbiji na kusababisha vifo vya watu kiasi hamsini na watano.

Mafuriko hayo yameharibu miji na mazao.

Watu kadhaa wametoweka katika mataifa hayo matatu ya kusini mwa Afrika.

Wakuu wa serikali wametahadharisha huenda kukatokea janga la kibinadamu hasa katika mji mkuu wa Angola, Luanda na maeneo ya karibu ambayo yameathirika zaidi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com