LONDON: Chembe za kinuklia katika mwili wa jasusi wa zamani | Habari za Ulimwengu | DW | 25.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Chembe za kinuklia katika mwili wa jasusi wa zamani

Maafisa wa Kingereza wanaochunguza kifo cha jasusi wa zamani wa Urussi,Alexander Litvinenko, wanasema kiasi kikubwa cha minunurisho ya kinuklia ya sumu kali sana ya polonium 210 imekutikana katika mwili wake.Litvinenko alifariki siku ya Alkhamisi katika hospitali mjini London,baada ya kuanza kuugua majuma matatu ya nyuma.Wachunguzi wanasema wamegundua pia chembe za minunurisho ya kinuklia nyumbani kwake, kwenye mkahawa na hoteli ambako inasemekana kuwa alikutana na watu fulani.Matamshi ya mwisho yaliotolewa na Litvinenko siku chache kabla ya kufariki,yalisomwa na rafiki yake Alexander Goldfarb mbele ya waandishi wa habari mjini London.Katika taarifa hiyo Litvinenko ametuhumu kuwa rais Vladimir Putin wa Urussi ndio alitoa amri ya kumuua.Lakini Putin akihudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Urussi mjini Helsinki,Finnland amekanusha kuhusika kwa njia yo yote ile.Litvinenko alikuwa akichunguza mauaji ya mwandishi wa habari wa Kirussi Anna Politkovskaya yaliotokea mwezi uliopita mjini Moscow.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com