LISBON: Rais Putin tayari kwa mazungumzo na Umoja wa Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 25.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LISBON: Rais Putin tayari kwa mazungumzo na Umoja wa Ulaya

Rais Vladimir Putin wa Urusi leo anatarajiwa kuwasili mjini Lisbon ambapo atafanya mazungumzo na viongozi wa Ureno kabla ya mkutano wake na viongozi wa Umoja wa Ulaya hapo kesho .

Wadadisi wamesema mkutano huo unaweza kukabiliwa na mvutano juu ya masuala ya nishati na biashara.

Rais Putin anaetarajiwa kuwasili Ureno leo alasiri,atakutana na rais Anibal Silva pamoja waziri mkuu wa nchi hiyo Jose Socrates.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com