LIPUNGA.sakata ya mtoto wa Malawi anayetarajiwa kulelewa na Madonna yazusha mvutano mpya | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LIPUNGA.sakata ya mtoto wa Malawi anayetarajiwa kulelewa na Madonna yazusha mvutano mpya

Baba wa mtoto anayetarajiwa kulelewa na mwanamuziki wa kimataifa Madonna kutoka nchini Malawi ameongeza mvutano mpya katika sakata hiyo iliyogonga vyombo vya habari duniani kote.

Baba huyo sasa anasema kuwa hakuwa na nia wala matarajio ya kumgawa mwanawe kwa mwanamuziki huyo ila makubaliano yalikuwa tu Madonna angemlea mtoto huyo kwa niaba ya baba huyo.

Ugeugeu huo umesababisha muelekeo mpya katika sakata inayo muhusu mtoto wa kimalawi ambae mwanamuziki maarufu duniani anatarajia kumlea na kumfanya mwana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com